Wednesday, October 12, 2016

UBORESHAJI

Shirika la mapato Tanzania{TRA} laanza uboreshaji wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi(TIN NUMBER),ili kuwezesha walipakodi kuwa na namba moja ya utambulisho,ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za mlipa kodi.
Awali mlipa kodi mmoja alikuwa akimiliki( TIN) zaidi ya moja kama ya biashara,leseni ya udereva,n.k ambazo zilikuwa zikitolewa tofauti kutokana na matumizi husika.Ubadiishaji na uboreshaji huu umeanza katika jiji la Dar es salaam na baadaye kwenda mikoa ya nchi nzima.Mpaka sasa timu ya TRA yaendelea na ziara ya kutoa elimu kwa mlipa kodi,ili wawe na elimu tosha juu ya tozo za kodi.
TRA KWA MAENDELEO YA TAIFA

No comments:

Post a Comment